Jumatatu 28 Aprili 2025 - 20:01
Msighafilike mkaacha kusoma Swala ya Mtume (s.a.w.w.)

Ayatullah Bahjat anasema kwamba "kumswalia Mtume" ndiyo njia bora zaidi ya kuimarisha urafiki na upendo kwa Mwenyezi Mungu. Yeye anasisitiza kuwa, kwa moyo wa mapenzi na shauku, mtu ajishughulishe na dhikri ya kumswalia Mtume, ili aweze kushuhudia kuongezeka mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, je, unatafuta njia ya kuongeza mapenzi ya Mwenyezi Mungu ndani ya moyo wako? Ayatullah Bahjat anaeleza kuwa "kumswalia Mtume kwa mapenzi" ndiyo ufunguo wa mafungamano haya. Kwa kumswalia Mtume, unajenga mafungamano ya kina zaidi na Mola wako Mpendwa.

Maneno ya Ayatullah Bahjat - Quddisa Sirruh:

“Mtu anayetaka urafiki na mapenzi yake yazidi, katika nyiradi, adaab na ibada mbalimbali, hakuna jambo lililo rahisi zaidi kuliko kusoma kumswalia Mtume mara nyingi zaidi;

Mtu atakapo mswalia Mtume kwa moyo wa mapenzi, ataelewa namna mapenzi yake yanavyozidi kwake; lakini kwa sharti la kuwa na imani sahihi, yaani, atambue kwamba dhikri hiyo inamvuta kumuelekeza kwa Mola wake na Mpenzi wake wa kweli.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha